Tuesday 24 June 2014

Mambo mazito



  • Serikali yasema misamaha ya kodi imetosha
  • CAG kuchunguza iliyoingiwa na wawekezaji
  • Kodi ya PAYEE, ukomo wa mikweche palepale

SERIKALI imesema haitapunguza zaidi kodi kwenye mishahara ya wafanyakazi (PAYE) kwa sasa kutokana na ongezeko la mishahara lililofanywa kwa wafanyakazi wa sekta ya umma hivi karibuni.

Aidha serikali imesema umri wa magari yatakayoruhusiwa kisheria kuingizwa nchini utaendelea kuwa miaka minane badala ya 10 kama ilivyopendekezwa kwenye bajeti ya serikali.
Msimamo huo wa serikali ulielezwa jana na Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum alipokuwa akijibu hoja za wabunge waliochangia bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2014/2015.
Saada alisema kiwango kilichopunguzwa na serikali katika kodi ya mishahara ya wafanyakazi ni kidogo, lakini mfanyakazi anaweza kupata nafuu kutokana na ongezeko la mishahara.
Alisema lengo la serikali ni kuendeleza kupunguza kodi hiyo hadi ifikie tarakimu moja kama ilivyopendekezwa na wabunge wakati wakichangia bajeti hiyo.
"Tumeshusha kodi kwa asilimia moja kutoka asilimia 13 hadi 12, lakini wakati huo huo serikali imepandisha mishahara kwa kiwango ambacho kitampa nafuu kidogo mfanyakazi na kikubwa kuliko kodi anayokatwa,"alisema.
Waziri Mkuya pia alisema uamuzi wa kupunguza umri wa magari yanayoletwa nchini, umezingatia mambo mengi ya msingi, ikiwa ni pamoja na kuiepusha Tanzania kuwa jalala la magari chakavu.
Alisema kwa kuagiza magari yaliyotumika kwa miaka minane, matumizi ya serikali yatapungua na gharama za kununulia gari zitabaki zilezile kama zinazotumika kwa magari yaliyotumika kwa miaka 10.
"Mheshimiwa Spika, Tanzania imegeuzwa dampo, watengenezaji wa magari wanasubiri jinsi ya kucheza na bei," alisema.
Akitoa mfano, Waziri Saada alisema mfanyabiashara mmoja wa Tanzania ameingiza nchini magari 1,000, lakini ameshindwa kuyalipia kodi na tayari Mamlaka ya Kodi ya Mapato nchini (TRA), imeanza kuyapiga mnada.
Waziri Saada alisema kutokana na misamaha ya kodi kuwa wimbo wa Taifa bungeni, serikali imeshaanza kuchukua hatua za kuifuta ile isiyokuwa na tija na aliwataka wabunge wapitishe mswada wa fedha utakaowasilishwa bungeni hivi karibuni.
Apangua madai ya Kamati ya Chenge
Saada alikanusha madai ya Kamati ya Bajeti ya Bunge kuwa serikali haitaki kufuata ushauri wa kubuni vyanzo vingine vya mapato na kusikiliza ushauri inaopewa. Imesema siku zote serikali ni sikivu na itaendelea kuufanyiakazi ushauri wa kamati hiyo.
Waziri huyo alisema deni la taifa halipaswi kuitwa adui wa bajeti na haliwezi kuifanya serikali iache kukopa.
Alisema ukubwa wa deni hilo unatokana na madeni yaliyokopwa miaka zaidi ya 40 na 50 iliyopita na baadhi yameshaanza kulipwa na serikali. Alisema serikali itaendelea kukopa lakini kwa kuzingatia sheria na kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
"Deni la taifa haliepukiki, lazima tuendelee kukopa lakini tutakuwa waangalifu na kuzingatia sheria,"alisema.
Waziri Saada alisema pia kuwa serikali itakuwa makini katika kulipa madeni ya wazabuni kwa vile baadhi yamebainika kuwa ni hewa na yamekuwa yakiitia hasara serikali.
Alisema kuanzia sasa, serikali itaanza utaratibu wa kulipa madeni hayo baada ya kuyahakiki baada ya kubaini mengi yamekuwa yakigharimu fedha nyingi tofauti na viwango halisi ambavyo wazabuni wanaidai serikali.
"Kuna wakati lilikuja deni hazina la zaidi ya shilingi trilioni moja, lakini baada ya ukaguzi kufanyika, ilibainika kuwa deni hilo ni shilingi bilioni 143,"alisema.


Saada alisema kiwango kilichopunguzwa na serikali katika kodi ya mishahara ya wafanyakazi ni kidogo, lakini mfanyakazi anaweza kupata nafuu kutokana na ongezeko la mishahara.
Alisema lengo la serikali ni kuendelea kupunguza kodi hiyo hadi ifikie tarakimu moja kama ilivyopendekezwa na wabunge, wakati wakichangia bajeti hiyo.
“Tumeshusha kodi kwa asilimia moja kutoka asilimia 13 hadi 12, lakini wakati huo huo serikali imepandisha mishahara kwa kiwango ambacho kitampa nafuu kidogo mfanyakazi na kikubwa kuliko kodi anayokatwa,” alisema.
Waziri Saada alisema uamuzi wa kupunguza umri wa magari yanayoletwa nchini, umezingatia mambo mengi ya msingi, ikiwa pamoja na kuiepusha Tanzania kuwa jalala la magari chakavu.
Alisema kwa kuagiza magari yaliyotumika kwa miaka minane, matumizi ya serikali yatapungua na gharama za kununulia gari zitabaki zilezile kama zinazotumika kwa magari yaliyotumika kwa miaka 10.
“Mheshimiwa Spika, Tanzania imegeuzwa dampo. Watengenezaji  wa magari wanasubiri jinsi ya kucheza na bei,” alisema.
Waziri Saada alitoa mfano wa mfanyabiashara mmoja wa Tanzania ambaye ameingiza nchini magari 1,000, lakini ameshindwa kuyalipia kodi na tayari Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imeanza kuyapiga mnada.
Alisema kutokana na misamaha ya kodi kuwa wimbo wa taifa bungeni, serikali imeshaanza kuchukua hatua za kuifuta ile isiyokuwa na tija na aliwataka wabunge wapitishe muswada wa fedha utakaowasilishwa bungeni hivi karibuni.

Apangua madai ya Kamati ya Chenge
Saada alikanusha madai ya Kamati ya Bajeti ya Bunge kuwa serikali haitaki kufuata ushauri wa kubuni vyanzo vingine vya mapato na kusikiliza ushauri inaopewa. Alisema siku zote serikali ni sikivu na itaendelea kuufanyiakazi ushauri wa kamati hiyo.
Alisema deni la taifa halipaswi kuitwa adui wa bajeti na haliwezi kuifanya serikali iache kukopa na kwamba ukubwa wa deni hilo unatokana na madeni yaliyokopwa zaidi ya miaka 40 na 50 iliyopita na baadhi yameshaanza kulipwa na serikali. 
Hata hivyo, Saada alisisitiza kuwa serikali itaendelea kukopa lakini kwa kuzingatia sheria na mikopo hiyo itakuwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
“Deni la taifa haliepukiki, lazima tuendelee kukopa lakini tutakuwa waangalifu na kuzingatia sheria,”alisema.
Waziri Saada pia alisema serikali itakuwa makini katika kulipa madeni ya wazabuni kwa vile baadhi yamebainika kuwa ni hewa na yamekuwa yakiitia hasara serikali.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru