Saturday 7 June 2014

Mrema: Mimi sio kibaraka wa CCM


NA RODRICK MAKUNDI, MOSHI
MWENYEKITI wa Taifa wa TLP,  Augustine Lyatonga Mrema, amesema kamwe hana mpango wa kuunga mkono Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) na kusisitiza msimamo wake wa kutaka serikali mbili.
Mbali ya msimamo huo, Mrema amesema yeye sio kibaraka wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kama baadhi ya watu wanavyodai na kuwa: ìMimi nashangaa wakati wanasema mimi ni kibaraka wa CCM, tunaona wenyewe wameungana na CUF, sasa kweli kama sio wanatafuta maslahi binafsi hapa nini wanachokitengeneza kwa Watanzania?
Mrema alisema hayo jana alipozungumza na UHURU WIKENDI na kwamba  maridhiano hayawezi kupatikana kwa kususia vikao na kutaka wale wanaounda UKAWA, kuiheshimu kamati ya maridhiano yenye wajibu wa kusikiliza pande zinazotofautiana kwa hoja.
Mrema ambaye  ni Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), alisema anakusudia kuvikutanisha vyama vya siasa, ili kuzungumzia mustakabali mzima wa katiba mpya, sanjari na kusisitiza haja ya kukaa pamoja katika kukubaliana.†
Alisema licha ya kuwa mpinzani wa kweli na mwanasiasa mkongwe mwenye heshima ya pekee, haoni sababu ya kususia vikao vya bunge la katiba, kwa maelezo kuwa kitendo hicho sio uwakilishi wa wananchi bali kinalenga maslahi binafsi.
ìNinabaki kule bungeni...sasa ukisema nitoke nje nitakuwa namwakilisha nani, mimi ninatuhumiwa kwamba ni kibaraka wa CCM, lakini nataka niwahakikishie wapiga kura wangu kwamba mimi ni mpinzani wa kweli na sio kama wanavyosemaî, alisema.
Kwa mujibu wa Mrema, uzoefu  alionao kwenye siasa na mmoja wa watu waliofanya kazi usalama wa taifa, anatambua chimbuko la maridhiano ya awali ya kuwa na serikali mbili kwa misingi ya kiusalama na kamwe serikali tatu hazitakuwa na tija kwa Tanzania.
†Katika hatua nyingine, Mrema alisema wale wanaohoji kuwa yeye ni kibaraka wa CCM, wanapaswa kuulizwa kigezo waliochotumia kuungana na chama ambacho kimeshirikiana na CCM kule Zanzibar kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).
†ìMimi nashangaa wakati wanasema mimi ni kibaraka wa CCM tunaona wenyewe wameungana na CUF, sasa kweli kama sio wanatafuta maslahi binafsi hapa nini wanachokitendeneza kwa Watanzania? alihoji.
†Hata hivyo, aliwataka viongozi wa vyama vya upinzani waliounda UKAWA, kurudi nyuma na kumaliza kazi ya kuandaa katiba mpya, ambayo itakuwa dira ya kutafuta madaraka wanayopigania.
†Wakati huo huo, Mrema aliipongeza serikali kupitia Wizara ya Ujenzi kwa juhudi kubwa za uboreshaji wa barabara ambazo ni korofi  kwenye jimbo hilo na kusisitiza  nia yake ya kushirikiana na serikali iliyopo madarakani ya kuwaletea wananchi maendeleo.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru