Saturday, 18 April 2015

Atangaza kuwania ubunge Arumeru


NA SHAABAN MDOE, ARUMERU
JOTO la ubunge katika Jimbo la Arumeru Mashariki limezidi kupanda baada ya kada wa CCM wilayani humo, Elirehema Kaaya, kutangaza kuwania kiti cha ubunge katika uchaguzi wa mwaka huu.
Kaaya ambaye aliwahi kugombea nafasi hiyo mwaka 2005 na 2010, alisema juzi, kuwa hajakata tamaa kwa kuwa anaamini amejipanga kikamilifu.
Mtangaza nia huyo ambaye kwa sasa ni Ofisa Uhusiano wa Jiji la Mwanza, alisema kilichomsukuma kuwania ubunge ni pamoja na kusukumwa na dhamira ya kutatua kero mbalimbali za wakazi wa jimbo hilo, hususan migogoro ya ardhi.
Kaaya alisema jimbo hilo ni miongoni mwa majimbo yenye utajiri mkubwa ikiwa ni pamoja na vivutio vya utalii ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Arusha (ANAPA), lakini wananchi hawanufaiki na rasilimali hizo.
Alisema endapo Chama kitampa ridhaa kupeperusha bendera, ana uhakika wa kunyakua ushindi kwa kuwa amejipanga kutangaza sera zitakazowavutia wananchi.
ƬSitawapa pombe za viroba vijana, hususani wale wanaoendesha bodaboda. Nimejipanga kuwatangazia sera zitakazowavutia katika mikutano yangu,Ʈalisema Kaaya.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru