WATU wa Korea kila siku ya Aprili 15, husherehekea kuzaliwa kwa Rais Kim II Sung aliyezaliwa mwaka 1912 na kufariki mwaka 1994, ambapo huiita siku hiyo kama Siku ya Jua.
Rais huyo ndiye mwanzilishi wataifa la kijamaa la Korea, siku hiyo huitwa siku ya jua kutokana na kiongozi huyo kuwa na hadhi ya juu na mvuto mithiri ya jua.
Siku hiyo huwa ni siku ya kihistoria ambayo huonyesha zama mpya za historia ya mwanadamu, zama za uhuru iliyotokana na falsafa ya Juche, yenye kutambua kuwa nguvu ya watu ndiyo yenyekusukuma mafanikio.
Juche, iliweza kuwafikia mpaka moyoni mwa watu duniani, kukusanyika kusoma na kutapakaa kwa falsafa hiyo katika mataifa mengi kukiwa na taasisi zipatazo 1100 katika mataifa zaidi ya 100 ambapo katika kila bara kumekuwa na taasisi za kutoa elimu kuhusiana na falsafa ya Juche.
Rais Kim II Sung, alikuwa akiwapenda watu kwa mtazamo kuwa “Wananchi ndiyo Mungu wangu” ikiwa kama ndiyo kauli mbiu kwenye maisha yake kwa kuwa kila siku alikuwa akijichangaya na watu kwa ukaribu.
Alihakikisha watu wanapata huduma bure za afya na elimu katika taifa lote pamoja na kuondoa mfumo wa kodi kandamizi.
Akiwa kama Baba kwenye jamii ya Wakorea, aliweza kuhudumia familia yake kwa ukaribu , katika maisha yake wananchi walipenda kumuita “ Baba kiongozi” kuliko jina la cheo chake alichokuwa nacho.
Pia, alikuwa mwenye upendo kwa wageni bila kujali mataifa yao, falsafa, mitizamo ya kisiasa na imani za kidini.
IFUTAYO NI MIFANO THABITI.
Septemba 1964, Rais wa Kituo cha Redio cha Guinea alipata ugonjwa wa kuambikizwa alipokuwa ameitembelea Korea akiwa kama kiongozi wa msafara wa waandishi wa habari aliokuja nao.
Baada ya kupewa taarifa hiyo, Kim II Sung alitoa amri ya kutibiwa kwa kiongozi huyo kwa gharama zozote huku jopo la madaktari waliobobea wakipelekwa kumtibu.
Aliweza kufanyiwa upasuaji kwa kipindi cha masaa saba pamoja na kuwekewa damu alipokuwa amelezwa hospitalini.
Rais Kim II Sung alihakikisha kiongozi huyo anapatiwa tiba bora, ambapo wakati aliporejeshwa nchini Gunea alisafirishwa kwa ndege ya Korea akiongoza na jopo la madaktari.
Kreisky, Kansela na Mwenyekiti wa zamani wa chama cha kijamaa cha Austria alikuwa hawezi kutembea kutokana na kukabiliwa na maradhi.
Rais Kim II Sung, aliwatuma jopo la madaktari kutoka Korea kwenda Austria wakiwa na madawa ghali aina ya Koryo na hatimae waliweza kumtibu Kiongozi huyo.
Kim II Sung, wakati wa uhai wake kutokana na ukarimu wake aliweza kuwatembelea watu kutoka mataifa ya kigeni zaidi ya 70,000 wakiwemo, Stalin, Julius Nyerere kutoka Tanzania, Mao ze Dong, Zhou Enlai, Fidel Castro, Norodom Shehanouk, Ho Chi Minh, Tito na Lasana Konte.
Baadhi yawageni walipenda ukarimu wake na walitamani kurudi tena kumtembelea ambao katia yao alikuwa Luise Rinser, mwandishi wa vitabu kutoka Ujerumani.
Wakati alipokutana na Kim II Sung, waliamini kuwa ni kama Mungu ambapo Muhubiri kutoka Marekani Billy Graham alisema taifa la Korea linaongozwa na kiongozi ambaye Mungu amelifanikisha.
Wakati rais Kim II Sung, alipofariki Julai 1994, watu wengi duniani walihisi mbingu zimeanguka huku jua likizama ingawa jua lilikuwa likiangaza.
Mwili wake umehifadhiwa katika Jengo la Kumsusan, lijulikanalo kama Nyumba ya Jua. Watu wa Korea wanaikumbuka April 15 kama siku ya kuzaliwa kwake.
Kauli mbiu ya katifa la Korea ni “Kiongozi wetu mkuu, Komredi Kim II Sung, yupo nasi kila siku” na “Tuinue mikono yetu kuunga mkono fikra za kimapinduzi za Kiongozi wetu Komredi Kim II Sung!” huku picha yake ikipamba kwa tabasamu lake zuri.
Tamasha la Kirafiki la Mwezi Aprili la sanaa za kimataifa, hufanyika kuazimisha siku ya kuzaliwa kwake. Pamoja na maonyesho katika mlima Myohyang, zikionyeshwa zawadi zilizowasilishwa kwake baada ya kifo chake kutoka kwa viongozi wa mataifa ya kigeni, wanasiasa na wanajamii.
April 1995, mwaka mmoja baada ya kifo chake, tamasha la shujaa wa kabila la Jua lilifanyika Nigeria. Katika tamasha hilo mfalme wa jamii ya Ummuozzi alisema “Rais Kim II Sung, ni jua linaloangaza usawa wa ubinaadamu. Licha ya kufariki kwake, daima atakuwa nasi kama jua linavyoa angaza”
Kama Jua linavyoa angaza hivyo Rais Kim II Sun, ni moyo wa usawa kwa wanaadamu.
MANGYONGDAE
MANGYONGDAE ni mji aliozaliwa kiongozi mwanzilishi wa Taifa la kijamaa la Korea Kim II Sung Aprili 15, 1912.
Mji huo unajulikana zaidi kutokana na uzuri wake tangu enzi za Karne kutokana na kuzungukwa kwa mabonde na mlima mrefu wa Mangyong.
Katika mabonde hayo watu wanafurahia mandhari nzuri ya ndege wazungukao mabonde hayo, katika mji huo aliozaliwa Rais wa taifa la Korea unaendelewa kutunzwa kama hazina ya taifa.
Wageni wanashangaa na kuvutiwa namna nyumba ya kiongozi huyo ilivyokuwa ya kawaida ukilianganisha na makazi ya viongozi wengine ulimwenguni.
Kiuhalisia ilikuwa nyumba ya mtumishi kwenye mabonde na makaburi ya Bwanyenye katika mji wa Pyongyang.
Familia yao ilikuwa masikini sana kukidhi kugharamia nyumba ya namna hiyo iliyotokana na Babu yake mkubwa kuwa mtunza makaburi ya Bwanyenye na kumfanya aweze kuishi hapo.
Katika nyumba hiyo ndipo waliishi wazalendo waliojitolea maisha yao kulitumika taifa lao kwa kizazi hadi kizazi.
Kim Ung U, ambaye ni Babu yake mzaa babu wa Kim II Sun, aliongoza kuizamisha meli ya General Sherman uliyofanyiwa ukarabati na kuitwa Shenandoah, meli hiyo ya Marekani iliivamia Korea katika kipindi cha katikati ya Karne 19.
Mababu wa rais wa taifa la Korea walishirikiana kwa juhudi za dhati kupitia shughuli za kimapinduzi kwa watoto na wajukuu zao wakiwa kama wakulima wa kawaida.
Nyumba hiyo pia ilikuwa makazi ya Baba yake Kim Hyong Jik, kiongozi imara aliyepinga uvamizi wa Japan katika taifa la Korea, Mjomba wake Kim Hyong Gwon na mdogo wake Kim Chol Ju, walijitolea maisha yao kwa ajili ya kufanikisha harakati za mapinduzi kisha kujipatia uhuru.
Mama yake Kim Kang Pan Sok, kiongozi shujaa aliyewaongoza wanawake wa Korea pia aliishi katika nyumba hiyo kwa kipindi kifupi.
Ndani ya nyumba hiyo kuna dawati pamoja na jiwe la wino lililokuwa likitumiwa na Kim II Sung wakati akiwa shuleni, pamoja na meza, ubao wa kuchorea, chombo cha kubebea moto, jembe, mkeka na kibao cha kushonea.
Aidha kuna chungu cha kuwekea maji hivyo maisha ya wazazi wa Rais huyo yalikuwa ni masikini hadi kufikia hatua ya kushindwa kununua jagi au ndoo za kisasa wakati huo za kutunzia maji.
Kutokana na mfumo huo wa maisha, babu na wazazi wa kiongozi huyo walimfundisha namna ya kuishi maisha ya kizalendo kulingana na mwenendo wa familia ya Mangyongdae waliokuwa tayari kufariki pasipo kusita kwa manufaa ya taifa.
Uwanja wa mieleka, eneo la kusomea pamoja na mwamba mithiri ya manoali waliokuwa wakitumia kucheza wakati wakiwa askari ambapo Kim II Sun hamasa za kishujaa dhidi ya ufedhuri wa Japan bado vinaendelea kutunzwa.
Kim II Sung, aliondoka nyumbani baada ya baba yake alipoanzisha harakati za kupigania uhuru wa taifa hilo mwaka 1923.
Akiwa na umri wa miaka 11 alisafiri kwa miguu umbali wa kilometa 250, akitokea Kaskazini Mashariki ya China kwenda Mangyongdae kujifunza zaidi uhalisia wa taifa lake akiwa peke yake.
Januari 25, 1925, akiwa anasoma nchini kwake, alipewa taarifa yakuwa baba yake amekamatwa na askari wa Japan hivyo aliondoka Mongyongdae na kuapa kuwa hatorudi katika ardhi hiyo mpaka atakapo likomboa taifa lake.
Baada ya miaka 20, alirejea tena na kuanzisha harakati za mapambano dhidi ya unyonyaji uliokuwa ukifanywa na Japan na kufanikisha kulikomboa taifa hilo Agosti 15, 1945.
Akiwa amerejea kwa mafanikio alitembelea kiwanda cha chuma cha Kangson (Kwa sasa Chollima Steel Complex) kwa dhamira ya kuijenga Korea mpya licha ya njia ya kiwanda hicho ndiyo yakuelekea nyumbani kwao.
Baada ya kuanzisha chama cha Wafanyakazi wa Korea, Oktoba 10, 1945 akisaidiwa na wananchi awaliojawa na furaha katika mapokezi ya kihistoria yaliyofanyika Pyongyang, Oktoba 14, 1945, aliweza kuingia nyumbani kwao akitumia mlango uliojengwa kwa fito.
Bibi yake alimkimbilia alipofika barazani kwa kumbusu na kumlaki kwa kumwambia “kwanini umerejea nyumbani kwa kuwaacha nyuma baba na mama yako”.
Hali hiyo ilitokana na kuwa wanafamilia wengi waliiacha nyumba hiyo na kwenda kushiriki vita vya ukombozi lakini Kim II Sung ndiye pekee aliyerejea.
Tangu hapo, Rais Kim II Sung, popote pale anapouona mlango uliojengwa kwa fito hukumbuka ni wanafamilia wenzake wangapi waliotoka katika mlango wa aina hiyo na wangapi walirejea.
Kwa sasa Mangyongdae ni ardhi ya mapinduzia ya watu wa Korea iliyobarikiwa na maendeleo ya Dunia yaliyoamini katika falsafa ya Juche na kuhamasisha baada ya uhuru.
Wananchi wa Korea kutoka ndani na nje ya nchi pamoja na wageni wamekuwa wakitembelea eneo hilo kukusanya ujuzi wa Kiongozi huyo pamoja na kupanda miti na maua.
Zaidi ya watu milioni 120 wameshatembelea mji wa Mangyongdae katika kipindi cha miaka 60 iliyopita.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Toa Maoni Yako Kwa Uhuru