Na Antar Sangali, Zanzibar
Wataalamu 40 kutoka vyuo vikuu tisa vya Kiislamu vya Nchi za Afrika Mashariki na Malasyia watakutana Zanzibar kujadili maendeleo ya mitaala pamoja na kuangalia njia bora za kuwaepusha wanafunzi kutojihusiaha na matumizi mabaya ya mitandao ya jamii inayochangia kuwaingiza katika ugaidi na uhalifu.
Akizungumza mjini hapa, jana, Profesa Abdulrahaman Hikmany wa Chuo Kikuu cha Al Sumait cha Zanzibar, alisema mkutano huo wa kimataifa utaanza April 18 hadi 19, mwaka huu.
Profesa Hikmany alisema lengo la mkutano huo ni kuchambua maendeleo ya mitaala ya elimu kwa vyuo vikuu vya Afrika Mashariki na Kusini wa Afrika.
Alisema utandawazi kwa njia moja au nyingine una faida na hasara, na kutoa mfano kuwa binadamu hawezi kukatazwa asitumie kisu ila jambo la msingi kumpa njia kukitumia kwa tahadhari.
“Kusudio la mkutano huo ni kuibua mbinu mpya endelevu katika mitaala na kuelemisha vijana kuhusu madhara na taathira za za utandawazi na mawasiliano, simu na mitandao katika matumizi ya komyuta, tunachotaka wafahamu tija na na kama zake hakuna chema kisicho na athari. Ndiyo maana kuna wanaotumia dawa za kulevya licha ya hatari ya jambo hilo,îalisema.
Aidha alitaja teknolojia za mawasiliano kuwa zimerahisisha kazi za utafiti kufanyika muda mfupi na kwamba, eneo hilo limeathiri baadhi ya vijana kuitumia vibaya mitandao kinyume na mahitaji na kutumbukia katika matatizo ya uhalifu.
Mkutano huo umeandaliwa na Taasisi ya Kimataifa ya Fikra ya Kiislamu yenye makao yake nchini Malaysia. Vyuo vikuu vingine vitakavyoshiriki ni Chuo Kikuu cha Kiislam cha Morogoro, Chuo Kikuu cha Umma (Kenya), Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Abdulrahaman Al Smait (Zanzibar), Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Uganda, Chuo Kikuu cha Mussa Bin Bique (Msumbiji), Chuo Kikuu cha Kiislamu (Sudan Kusini), Chuo Kikuu cha Kiislamu (Malaysia) na Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) ambacho kitashiriki mkutano huo kama mtazamaji na mwalikwa.
Saturday, 18 April 2015
Watalaamu vyuo vya Kiislamu kukutana Z,bar
09:21
No comments
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Toa Maoni Yako Kwa Uhuru