Tuesday, 14 April 2015

TASAF haina dini wala siasa-Mwamanga


NA SOPHIA WAKATI,TANGA
MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF),Ladislaus Mwamanga, ameitaka jamii kuelewa kuwa chombo hicho ni cha serikali na hakina mwingiliano wa dini, wala itikadi yoyote ya kisiasa.
Alisema lengo la TASAF ni kuonyesha uwajibikaji na kuwezesha wananchi wote kuwa na maisha bora.
Mwamanga aliyasema hayo jana, mkoani hapa, alipokuwa akizindua kikao kilichojumuisha waandishi, waratibu, wahasibu na maofisa wanaofuatilia shughuli za mfuko huo.
Alisema serikali kupitia TASAF, imefanikiwa kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo ya wananchi, ambapo sasa imekuja na mpango kazi wa kunusuru kaya masikini, ili kuwezesha wananchi wote, hasa wa vijijini, kuwa na maisha bora.
“Hivi sasa tunatekeleza mpango wa TASAF awamu ya tatu, unaolenga kusaidia kaya masikini,wananchi wenye hali duni, ambao huwezeshwa kifedha, ili  wajitegemee,” alisema.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru