Na Angela Sebastian, Kyerwa
WACHIMBAJI wadogo wanaojihusisha na uchimbaji wa madini ya bati katika mgodi wa Nyaruzumbula, uliko kijijini Kabingo, wameiomba serikali kuwapatia ruzuku.
Lengo la ruzuku hiyo ni kutaka kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili, ikiwemo bei ndogo ya madini hayo na utoroshwaji unaofanywa na wananchi wasiokuwa wazalendo.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya, Luten Kanali Benedict Kitenga, mbele ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga, alipofanya ziara wilayani hapa.
Mwenyekiti wa wachimbaji hao, Theophily Rukanyanga, alitaja changamoto nyingine kuwa ni wachimbaji kufanywa chombo cha utafiti kwa ajiili ya wachimbaji wakubwa na wakishaibua eneo lenye madini, hufukuzwa na kupewa wachimbaji wakubwa.
Kitwanga alisema serikali imeamua kuhakikisha wachimbaji wasio rasmi kama hao wanarasimishwa kwa kupewa leseni itakayowafanya wachimbe kisasa na kufuata sheria na utaratibu.
Tuesday, 14 April 2015
Wachimbaji wadogo waomba ruzuku
08:23
No comments
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Toa Maoni Yako Kwa Uhuru