NA MWANDISHI WETU
WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi imesema inaendelea na ukaguzi wa vyama vya kijamii na kwamba vikibainika kukiuka matakwa ya kisheria, vitafutwa.
Taarifa iliyotumwa na Msemaji wa Wizara hiyo, Isaac Nantanga, kwa vyombo vya habari jana ilisema kutokana na orodha waliyo nayo, vyama 10,000 vya kijamii na taasisi za dini, vimesajiliwa katika wizara na kwama vitakavyofutwa ni vile ambavyo haviwasilishi taarifa za kila mwaka za ukaguzi wa hesabu zao.
Taarifa ilisema kama vyama hivyo havilipi ada ya kila mwaka, kama sheria inavyotaka ni lazima vitafutwa lakini kwa vile ambavyo vinatekeleza matakwa hayo ya kisheria, havitafutwa.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, orodha ya vyama vitakavyofutwa itatolewa kwa awamu, kuanzia wiki hii na kwa kuanzia itahusu vyama vilivyosajiliwa mkoni Dar es Salaam.
Aidha, ilisema kuwa ni vyema ikaeleweka kuwa zoezi linaloendelea kwa sasa halihusiani na taasisi zinazoelezewa kujiingiza katika masuala ya kisiasa na pia wizara haihusiki na usajili wa NGO.
Tuesday, 21 April 2015
Ukaguzi wa vyama vya hiari waanza rasmi
08:39
No comments
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Toa Maoni Yako Kwa Uhuru