Thursday 6 March 2014

Kalenga waaswa kutobadili msimamo


Na Mwandishi wetu, IRINGA
MWENYEKITI wa CCM wilaya ya Iringa Vijijini, Delfina Mtavalilo, amewataka wakazi wa jimbo la Kalenga wilaya ya Iringa Vijijini kutobadili msimamo wa kumchagua mgombea wa CCM kama walivyofanya mwaka 2010.
Delfina aliyasema hayo jana katika mkutano wa kampeni wa kumnadi mgombea wa CCM, Godfrey Mgimwa, uliofanyika katika Kijiji cha Kikombwe, jimboni Kalenga.
Alisema wakazi wa Kalenga ni vyema wakamchagua mgombea wa CCM, Godfrey katika uchaguzi unaotarajia kufanyika Machi 16, mwaka huu.
Alisema kwa kufanya hivyo watakuwa wameonyesha msimamo wa kukipenda Chama hicho.

“Mwaka 2010 katika uchaguzi mkuu mlionyesha msimamo wenu kwa kuifanya CCM ishinde katika nafasi ya rais, mbunge na diwani.
“Tunaomba katika uchaguzi huu mdogo pia muonyeshe msimamo huo huo,” alisema Delfina.
Alisema uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Machi 16, mwaka huu, si kwa ajili ya kuchagua Serikali, bali ni kujaza pengo lililoachwa wazi na mwana-CCM aliyekuwa anaendelea kutekeleza Ilani ya Chama.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru