Wednesday 12 March 2014

Wanaume walaghai kukiona


Na mwandishi wetu
SERIKALI mkoani Tabora imeazimia kuwashughulikia wanaume wote watakaobainika kulaghai wanafunzi wa shule za msingi au sekondari na kufanya nao ngono.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa, aliyasema hayo hivi karibuni kutokana na kushamiri kwa matukio ya ukatili na kuwanyanyasa watoto wa kike hivyo, kushindwa kupata haki ya kusoma.
Alisema kuna kila sababu ya kukabiliana na changamoto zozote zenye lengo la kumrudisha nyuma mtoto wa kike hususan kielimu na kwamba, jamii yote inapaswa kuwajibika.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru