Thursday 6 March 2014

Wana - Kalenga walonga


WAKAZI wa Kijiji cha Makongati, wamesema aliyekuwa mbunge wa jimbo la Kalenga mkoani Iringa marehemu Dk.William Mgimwa amefanya kazi kubwa ya kuleta maendeleo, hivyo kitakachofanyika ni kumchagua mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuziba nafasi hiyo.
Wakizungumza jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Makongati, kata ya Maboga mkoani Iringa, wakati wa kumnadi mgombea ubunge wa CCM, Godfrey Mgimwa, wananchi hao walisema wanaamini mbadala wa Dk.Mgimwa amepatikana ambaye ni Godfrey.
Akizungumza kwa niaba ya wakazi hao, mkazi wa Kijiji cha Makongati B, Uchungu Kilawa, alisema Dk. Mgimwa wakati wa uhai wake alifanya kazi kubwa ya kuleta maendeleo katika jimbo hilo na sasa amepatikana mgombea ambaye anaweza kuiendelea kazi hiyo.
“Mungu amesikia kilio chetu, maana Godfrey Mgimwa ataendelea kufanya kazi ya kuleta maendeleo katika jimbo letu, hatufanyi makosa siku ya uchaguzi,” alisema Kilawa.
Alisema baba yake Godfrey, Dk.Mgimwa alifanya kazi kubwa na hiyo imefanya wawe na moyo wa kumchagua mgombea huyo wa CCM.
Alisema mtangulizi wake alikuwa ni mtu wa msaada kwa wapiga ura wake, hali inayowashawishi pia kumchagua Godfrey ambaye wanaimani atafuata nyayo zake.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru