Tuesday 18 March 2014

Wanafunzi VETA waokoa Bilioni 1.4/-


NA MWANDISHI WETU
MAMLAKA ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) wilayani Makete, imeokoa zaidi ya sh. Bilioni 1.4 katika ujenzi na maboresho ya chuo hicho kwa kuwatumia wanafunzi na walimu kujenga miundombinu ya chuo hicho.
Wanafunzi hao na walimu, walijenga  mabweni na vyumba vya madarasa kama makandarasi wa ndani.
Mkurugenzi wa VETA mkoani Iringa, Monica Mbele, alisema kupitia wanafunzi, wameokoa gharama ya ujenzi na utengenezaji wa samani.
Monica ambaye alizungumza na mwandishi wa habari hii kuhusu mafanikio ya VETA hivi karibuni, alisema majengo yaliyojengwa yana kiwango cha juu, na samani zinazotumika chuoni hapo zimetengenezwa na wanafunzi.
Alisema chuo hicho kwa sasa kinauwezo wa kupokea wanafunzi 320 ambao watasoma kwa awamu mbili, mchana na jioni.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru