Monday 17 March 2014

Makonda aichana


CHADEMA
Na Mwandishi Wetu
KATIBU wa Uhamasishaji na Chipukizi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Paul Makonda, amesema CHADEMA haina uwezo wa kuongoza dola miaka 50 ijayo.
Amesema viongozi wa chama hicho ni tofauti na wa CCM na kwamba, wameshindwa kuongoza na kutenda haki kwenye baraza kivuli la mawaziri wanaloliongoza.
Makonda katika taarifa kwa vyombo vya habari aliyoitoa jana, alisema katika uchambuzi alioufanya amebaini udhaifu na uwezo mdogo wa uongozi ndani ya baraza kivuli la mawaziri linaloongozwa na CHADEMA.
Alisema uwezo alionao Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe ni mkubwa kuliko alionao Waziri Kivuli wa wizara hiyo, Godbless Lema.
Makonda alisema uwezo alionao Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, haufanani na wa Waziri Kivuli wa wizara hiyo, Mchungaji Peter Msigwa.
Alisema Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete, ana uwezo mkubwa wa kuongoza tofauti na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe.
Kwa mujibu wa Makonda, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, ana uwezo na uzoefu wa hali ya juu wa uongozi tofauti na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa.
Alisema Sekretarieti ya Chama iko imara kuliko ya CHADEMA ambayo imetawaliwa na majungu, ukabila na kuhamasisha vurugu nchini.
Makonda alisema uwezo wa viongozi hupimwa kwa kutathmini uwezo, maarifa na uzoefu, ambayo inaonyesha CCM itaendelea kuwa bora nchini kuliko vyama vingine vyote.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru