Wednesday 19 March 2014

‘Rasimu ya Katiba ijadiliwe kwa makini’


NA Mwandishi wetu, DODOMA
MAKAMU Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mkuu mstaafu Augustino Ramadhani, amewataka wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kuijadili kwa umakini Rasimu ya Katiba kwa maslahi ya wananchi.


Jaji Ramadhani alisema hayo bungeni juzi, baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, kuwasilisha rasimu hiyo.
Alisema wananchi wanasubiri kwa hamu kuona wanapata katiba yenye maslahi kwao, hivyo ni jukumu la wajumbe kuhakikisha kazi inafanyika kwa umakini.
“Wananchi wana matumaini mtaifanya kazi kwa uadilifu na kwa maslahi ya taifa, si itikadi za vyama na ubinafsi. Nawasihi kuhakikisha katiba itakayopatikana itumike kwa zaidi ya miaka hata 50,” alisema.
Alisema katiba ni sheria mama, inayojenga misingi na mustakabali wa wananchi kwa jumla, hivyo ni lazima umakini uwepo katika kuiandika.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru