NA ABOUD MAHMOUD,ZANZIBAR
RAIS mstaafu wa Zanzibar, Dk. Salmin Amour amewahimiza vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kusimama kidete ili kulinda uhuru na Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na kuyakataa mawazo ya kinyang’au yenye malengo ya kutaka kukumbatia upya ukoloni.
Dk. Salmim alitoa kauli hiyo nyumbani kwake Migombani mara baada ya Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar, Shaka Hamdu Shaka kuhitimisha ziara ya siku sita katika mikoa mitatu ya Unguja.
Alisema uhuru na ukombozi hupatikana mara moja, hivyo kuwataka vijana wa kizazi kipya kubeba dhamana ya kuulinda uhuru ulioletwa na vyama vya TANU pamoja na kuyatetea kwa nguvu zao zote Mapinduzi ya ASP.
"Pamoja na kuwa kazi ya UVCCM ni kukiimarisha chama chetu, agizo langu kwenu ni kuwa mjipange kupambana na manyangíau wenye nia ya kupora uhuru wenu na kuyapoteza Mapinduzi ya Zanzibar,î alisema Dk. Salmin.
Alisema nchi za Afrika, Marekani na Ulaya watu walikataa kutawaliwa na kwamba vijana ndiyo walijitolea maisha yao kupinga ukoloni hadi pale uhuru kamili, dhuluma na manyanyaso yalipomalizika na wananchi kujitawaliwa wenyewe.
Dk. Salmin alitoa mfano wa viongozi kama kina Mahatma Gandhi wa India, Martin Luther King Jr. wa Marekani, Vladimir Lenin na Max kuwa kati ya viongozi waiokataa kutawaliwa hadi walipojikomboa na kupata uhuru, hivyo ni muhimu kuwekatahadhari dhidi ya manyangíau wanaokumbatia wakoloni.
Aidha, alisema barani Afrika, kamati iliyosimamia ukombozi ya PAFMECA ilisimamia ukombozi na uhuru wa Waafrika hadi ukapatikana, huku akitaja uhuru ni thamani inayojenga utu na heshima yenye gharama.
Akizuingumzia mfumo wa vyama vingi nchini, alisema vijana hawana budi kufahamu kuwa demokrasia hiyo isiwasahaulishe na kupuuzia nguvu za wazee wao waliopigania uhuru hadi Tanganyika na Zanzibar kuwa huru.
ìDemokrasia ya vyama vingi ni jambo zuri... vyama hushinda kwa sera badala ya shari na mivutano, hatua hiyo isitoe kibali ya kuwakumbatia upya wakoloni ili kutimiza malengo yao, kwa hilo wala msije mkakubali na kuliruhusu,” alisisitiza.
Hata hivyo, Rais huyo mstaafu wa Zanzibar aliwaambia vijana hao kwamba kabla ya kupatikana kwa Uhuru na kupita kwa Mapinduzi, waafrika walinyimwa fursa ya kupata elimu, huduma muhimu za jamii, hivyo dunia inaweza kuwashangaa ikiwa watakubali kurejea tulikotoka.
Dk. Salmin aliwaeleza vijana hao kuwa ushindi wa CCM lazima utokane na nguvu ya umoja miongoni mwao, na kwamba wazidi kuendana pamoja na kuwa tayari kukubali kukosoa, kukosolewa na kuvumiliana.
Alitumia nafsi hiyo kuelezea kuhusu afya yake, ambapo alisema hivi sasa imeimarika kuliko awali, na kwamba amepata nafuu huku akiwa tayari wakati wowote kushirikina na wenzake katika kuiendeleza CCM.
“Sijambo... hivi sasa namshukuru Mungu mtukufu, hali yangu ya sasa si ile ya wakati ule, nazidi kupata faraja kuona mnanikumbuka na kunitembelea, hidaya na tunu muungwana akipewa hupokea na kutakiwa awe ni mwenye kushukuru,” alisema Dk. Salmin.
Tuesday, 2 July 2013
Dk. Salmin aihimiza UVCCM kukataa ukoloni
09:21
No comments
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Toa Maoni Yako Kwa Uhuru