Monday 8 July 2013

Magufuli aibukia daraja la Mbutu


Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Ujenzi Dk. John Magufuli, amefanya ziara ya ghafla kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja la Mbutu wilayani Igunga, Tabora.

Daraja hilo linajengwa katika barabara ya Igunga – Manonga, ambapo kwa muda mrefu limekuwa kero kwa wakazi wa Igunga.
Akizungumza katika eneo la ujenzi, Dk. Magufuli alimtahadharisha mkandarasi
kuwa hatakuwa tayari kupokea visingizio vyovyote vitakavyodai kusababisha kuchelewa kukamilika kwa mradi huo.
Daraja hilo lenye urefu wa mita 46 na tuta la urefu wa kilomita tatu, linajumuisha ujenzi wa makalvati makubwa saba na mradi unatekelezwa na muungano wa wakandarasi wazalendo 13 kwa gharama ya sh. bilioni 10.456.
Mkataba wa ujenzi wa daraja la Mbutu ulisainiwa Aprili, 2012 na umepangwa kukamilika kabla ya mwishoni mwa mwaka huu.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru