KAMPUNI ya Oryx Energy imeanza utaratibu wa kuwapelekea wateja gesi majumbani, ili kurahisisha upatikaji wa bidhaa hiyo.
Huduma hiyo inayojulikana ‘piga uletewe’ inatolewa bure kwa mteja anayetakiwa kupiga simu kwa wakala aliye jirani na eneo analoishi.
Meneja wa Matangazo na Bidhaa wa kampuni hiyo, Peter Ndomba, alisema huduma hiyo inatolewa bure na mteja atakayetozwa gharama za usafirishaji atoe taarifa kwa kampuni hiyo.
Alisema mawakala wameelimishwa kuhusu utoaji huduma hiyo na kwamba, mteja anatakiwa kuchukua namba ya simu ya wakala ili aweze kumpigia anapohitaji huduma.
“Huduma hii hutolewa bure, wakala atakayemtoza mteja gharama za usafirishaji akibainika atafutiwa mkataba,” alisema.
Alisema utaratibu huo hutumika katika nchi mbalimbali duniani, kama vile Afrika Kusini na India, na unalenga kuondoa maduka ya gesi katika maeneo ambayo si salama kwa biashara hiyo.
Monday, 8 July 2013
Oryx kupeleka gesi majumbani
08:28
No comments
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Toa Maoni Yako Kwa Uhuru