Sunday 7 July 2013

Sabasaba ‘yamkuna’ Dk. Sheni


Na Mwandishi Wetu
RAIS wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Sheni, ameyasifu maonyesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika jijini Dar es Salaam, kuwa yametoa nafasi kubwa kwa wajasiriamali wadogo.
Dk. Sheni, aliyasema hayo baada ya kutembelea mabanda ya maonyesho hayo, katika viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam jana, alipozungumza na waandishi wa habari.

Alisema mwaka huu yamefana zaidi ikilinganishwa na miaka iliyopita.
Dk. Sheni alisema kuna mafanikio makubwa, na hiyo inatokana na maandalizi mazuri yaliyofanyika.
Alisema pia yametoa fursa kwa washiriki kutoka sehemu tofauti za Tanzania, na hususan wajasiriamali wadogo.
Alisema mbali ya wajasiriamali, pia ushiriki wa kampuni mbalimbali zipatazo 1,600 kutoka nchi 32, kumeleta changamoto kwa wafanyabiashara wa nchini.
Hata hivyo, alitoa wito kwa Watanzania kuzithamini bidhaa zinazotengenezwa nchini, badala ya zitokazo nje.
“Lazima tuthamini cha kwetu… thamini chako hadi usahau cha mwenzako,” alisema Dk. Sheni.
Wakati huo huo; Dk. Sheni alitoa wito kwa wanaotembelea maonyesho hayo, kutoishia kutazama tu, bali wanunue, wasome na kujielimisha zaidi kutokana na maonyesho hayo.
Mapema, Dk. Sheni alitembelea mabanda mbalimbali ya maonyesho na kupata maelezo juu ya bidhaa zinazotengezwa na kampuni za ndani na nje ya Tanzanian

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru