Wednesday 10 July 2013

Mary Mwanjelwa awafunda vijana


NA SOLOMON MWANSELE, MBEYA
 MBUNGE wa Viti Maalum (CCM), Dk.Mary Mwanjelwa, amewataka vijana wa jijini hapa, kutokubali kutumiwa na baadhi ya wanasiasa, kama ngazi ya kupata umaarufu.
Aliyasema hayo jana, alipokuwa akiwapokea vijana 69 wa CHADEMA, waliojiunga na CCM.
Alisema watu wanaosimama majukwaani  na kuanza kuwatukana viongozi wa serikali ni wazi hawatoshi kuwa viongozi, kwani hawawezi kuwa mfano mwema kwa jamii.
 Mbunge huyo aliwazindua vijana hao katika tawi la wakereketwa la Ng’osi, lililopo kata ya Mwakibete, jijini Mbeya.

Alisema huwezi kuwa kiongozi makini, halafu muda huo unakuwa kinara wa kuhamasisha wananchi kufanya vurugu.
Dk. Mary, alisema kiongozi maini, ni yule anayehamasisha wananchi kuchangia maendeleo sambamba na kulinda amani, mshikamano na utulivu.
“Tunalo tatizo la soko la ajira, hali hii inawafanya vijana wengi warande barabarani na mwisho wa siku hujikuta wakitumiwa vibaya na baadhi ya wanasiasa wenye maslahi yao binafsi na siyo ya Watanzania,” alisema Dk.Mary.
Hata hivyo, alisema hiyo isiwe sababu ya kuwafanya wawe watumwa wa watu hao.
Alisema CCM ndio iliyoshika dola na itaendelea kuwa hivyo kwa miaka mingi ijayo, kutokana na imani kubwa waliyoijenga kwa wananchi kuwa inaweza kuwa viongozi wake wanaweza kuwatumikia.
Aliwapongeza vijana hao kwa uamuzi wao sahihi waliouchukua wa kujiunga na CCM, kwani hawajafanya kosa na aliwasisitizia kuwa kamwe hawatajutia uamuzi huo.
 Mbunge huyo wa viti maalumu, aliwapongeza vijana hao wa tawi la Ng’osi kwa kukataa kuendelea kutumiwa vibaya na CHADEMA, na kuwataka vijana wengine jijini hapa, kuiga mfano wao.
Wakati huo huo; Mbunge huyo aliwakabidhi vijana hao sh. 100,000 kwa ajili ya kuwawezesha kufungua akaunti ya kikundi chaon

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru