PETER NKANDUZO, DACICO
POLISI Kanda Maalum ya Dar es Salaam, imewahakikishia ulinzi wakazi wote wakati wa kipindi cha sikukuu ya Eid Elftri, ambapo askari zaidi ya 120 wameongezwa.
Kamanda wa Kanda hiyo Suleiman Kova, jana alisema kuwa watu wasiwe na wasiwasi katika kipindi cha kuelekea sikukuu kwani wameshanza kuimarisha ulinzi.
“Waambieni waende wakanunue bidhaa zao bila kubughudhiwa na mtu yeyote kwakuwa tumejipanga vyema,” alisema Kova.
Kova alisema wataendelea kufanya misako na doria kwa muda wote ikiwa ni pamoja na kuwakamata wahalifu sugu.
Aidha, aliwataka wenye maduka kuhakikisha wanafunga taa za kutosha, kamera za CCTV na kuweka walinzi waaminifu ili kuhakikisha usalama wa maeneo yao ya kufanyia biashara.
Hata hivyo, Kamnada huyo, alisema wataendelea kushirikiana na jamii ili kuzuia wahalifu wakati wa sikukuu inayotarajiwa kufanyika Agosti 8, mwaka huu.
Alitoa wito kwa wakazi wa jijini humo kujiepusha na vitendo vya uvunjaji wa amani na kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwa kisingizio cha kuwa na hasira kali.
Monday, 29 July 2013
Ulinzi kuimarishwa sikukuu ya Eid Elftri
09:04
No comments
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Toa Maoni Yako Kwa Uhuru