Sunday 7 July 2013

Waliosoma Mkwawa kutunzwa


NA RABIA BAKARI
VIONGOZI waliowahi kusoma Shule ya Sekondari Mkwawa, mkoani Iringa, wanatarajiwa kuvishwa nishani na kupewa tunzo maalumu za kulitumikia taifa.
Nishani na tunzo hizo pia zitatolewa kwa watu mashuhuri waliopitia shuleni hapo tangu mwaka 1961, na ambao wamekuwa na mchango mkubwa katika ujenzi wa taifa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya hafla hiyo, Catherine Tenga, alisema
hafla hiyo itafanyika Agosti 9, mwaka huu, katika ukumbi wa Kamrimjee, Dar es Salaam.
Licha ya utoaji tunzo, alisema kutaanzishwa umoja, kujenga mtandao wa kusaidiana kibiashara na kuandaa mfumo maalumu wa mawasiliano.
Alisema siku hiyo inajumuisha wanafunzi waliosoma shuleni hapo kuanzia mwaka 1961 ilipoanzishwa na wanachuo walioanza mwaka 2005, wakati ilipobadilishwa na kuwa chuo.
Miongoni mwa viongozi hao ni Profesa Tolly Mbwette, Profesa John Nkoma, Joseph Mungai, Maokola Majogo na Pindi Chana.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru