Tuesday 2 July 2013

JK, Obama waonyesha kiwango

RAIS Jakaya Kikwete na Rais wa Marekani, Barack Obama wakionyesha umahiri wa kusakata kabumbu. Hapa JK akipiga danadana kuonyesha yuko vizuri wakati walipotembelea mradi wa kuzalisha umeme wa Symbion uliopo Ubungo, Dar es Salaam.
NAJIBU MAPIGO: Rais Obama naye akionyesha kiwango cha kusakata kabumbu kwa kupiga danadana kwa kichwa. Mpira huo uliokuwa kivutio kikubwa kutokana na kuzalisha umeme.

HUJAMBO KOMREDI: Rais Obama akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, baada ya kutambulishwa na Rais Kikwete.
TUPO PAMOJA: Rais Obama akimweleza jambo Maswi huku Rais Kikwete, Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecki Sadiki wakisikiliza.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru