Sunday 7 July 2013

Wapenzi wanaswa na dawa za kulevya


NA MWANDISHI WETU
POLISI Kikosi cha Dawa za Kulevya inawashikilia wapenzi Ramadhani Shani na Pamela Msaki, wakituhumiwa kukamatwa na dawa za kulevya.
Wapenzi hao walikamatwa juzi, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam, wakiwa na kilo mbili za dawa za kulevya zenye thamani ya sh. milioni 90.
Akizungumza kwa simu jana, Kamanda wa kikosi hicho, Godfrey Nzowa, alisema walikuwa wanataka kusafiri kwenda China kwa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia.
Nzowa alisema polisi waliwatilia shaka na baada ya kupekuliwa kila mmoja alikutwa na kilo moja ya dawa za kulevya walizokuwa wameziweka kwenye begi zikiwa zimepakwa kahawa.
“Tunawashikilia na kuwahoji wapenzi wawili ambao walikutwa na dawa za kulevya, wakitaka kuzipeleka China,” alisema.
Nzowa alisema Shani alikutwa na hati ya kusafiria yenye namba 427507, iliyotolewa Agosti 29, mwaka 2010 na Pamela alikuwa na hati yenye namba AB 2011609 iliyotolewa Machi 27, 2007.
Alisema wapenzi hao watafikishwa mahakamani wakati wowote baada ya upelelezi kukamilika


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru