Monday 8 July 2013

TRA yasisitiza matumizi ya mashine kutoa risiti


MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imesema matumizi ya mashine za kielektroniki ni matakwa ya sheria na si mpango uliowekwa na mamlaka hiyo.
Imesema licha ya kuisaidia serikali kukusanya kodi sahihi, mashine hizo pia humwezesha mfanyabiashara kuweka kumbukumbu za kila siku.
Kaimu Mkurugenzi wa Fedha wa TRA, Rukia Adamu, alisema hayo  alipozungumzia mafanikio ya matumizi ya mashine hizo kwa wafanyabiashara wenye mauzo ya sh. 40,000 kwa siku. Uzinduzi wa matumizi ya mashine hizo ulifanyika Mei 15, mwaka huu.
Rukia aliwataka wafanyabiashara wote wasiosajiliwa kulipa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kutumia mashine hizo kwa hiari bila kusubiri kushurutishwa.
Alisema wapo baadhi ya wafanyabiashara wanaosita kutumia mashine hizo kutoa risiti.
Rukia akizungumzia malalamiko kuhusu baadhi ya wafanyabiashara katika maonyesho kutokutoa risiti kwa bidhaa wanazouza, alikiri kuwa hilo ni changamoto kwao.
Alisema kwa wafanyabiashara wa nje ya nchi, kuna takwimu zinazoonyesha bidhaa walizoingiza, hivyo baada ya maonyesho watalipa kodi kama kawaida.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru