Wednesday 10 July 2013

Rooney ampa raha Moyes


LONDON, England
WAYNE Rooney juzi alinogesha mazoezi ya Manchester United mbele ya bosi wake mpya David Moyes kwenye uwanja wa Carrington.
Kocha huyo alivutiwa na kiwango chake na mara kadhaa alionekana akitaniana naye pamoja na wachezaji wengine.
Rooney, amekata mzizi wa fitina baada ya klabu za Arsenal na Chelsea zilizokuwa zikimuwinda kwa nguvu kutaka saini yake majira ya kiangazi.
Nguli huyo amepaa na kikosi cha United katika ziara ya siku 21 ya kimichezo katika Bangkok, Sydney, Japan na Hong Kong.
Mkurugenzi Mtendaji wa United, Richard Arnold, alisisitiza kuwa Moyes atapata ushirikiano mkubwa wa kujenga timu imara kwa ajili ya msimu ujao.
"Jambo la kwanza kwangu ni kushinda kila mchezo ingawa nina changamoto mbele ya mtangulizi wangu Sir Alex Ferguson," alisema Moyes.
Kocha huyo ametwaa mikoba ya Ferguson aliyeng'atuka muda mfupi baada ya kuipa Man United ubingwa wa Ligi Kuu England.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru