Thursday, 21 August 2014

JK azindua huduma ya afya mtandao


NA LATIFA GANZEL, MOROGORO
RAIS Jakaya Kikwete  amezindua mradi mpya wa huduma  ya afya kwa njia ya mtandao (Telemedicine) katika kituo cha afya  cha Mwaya, wilayani Ulanga.
Mradi huo ni moja ya utekelezaji wa sera ya afya ya mwaka 2007 na una lengo la kuboresha huduma za afya vijijini ili kupunguza vifo vya watoto wenye umri chini ya imaka mitano na wajawazito.
Rais alisema huduma hizo zitasaidia kutatua matatizo yaliyoshindikana katika zahanati na kwamba watahakikisha huduam zote muhimu zinakuwepo kama ya upasuaji.
Pia aliaidi kushughulikia tatizo la soko la mpunga katika wilaya hiyo. Alisema serikali itatafuta masoko ya mazao ya chakula nje ya nchi ili kusaidia wakulima kuuza kwa tija.
“Nitahakikisha tunatafuta soko la mazao ya chakula nje ya nchi ambapo nilikwishawaagiza mawaziri nchi ya Sudan Kusini kuyatafuta, jambo litakalowezesha wakulima kuuza kwa faida,”alisema.
Wakati huo huo, Rais Kikwete jana litarajiwa kuzindua kivuko cha mto Kilombero kinachounganisha wakazi wa miji ya Ifakara na Mahenge.
Hivi karibuni abiria waliokuwa wakivuka kwa kutumia kivuko cha mto huo walinusurika baada ya kutokea hitilafu ambapo kilikwenda kuvuka katika kingo za daraja hilo linalojengwa.
Rais Kikwete yuko mkoani Morogoro kwa ziara ya kikazi ambapo atakagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa mkoani hapa.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru