Tuesday, 26 August 2014

Sherehe za kutunukiwa kamisheni maofisa wa Jeshi, Monduli.

Amiri Jeshi Mkuu, Rais Dkt. Jakaya Kikwete akisalimiana na mkuu wa majeshi wa kwanza Mzalendo Jenerali Mirisho Sarakikya muda mfupi baada ya kuwasili katika Chuo cha Jeshi Monduli, tayari kwa kutunuku kamisheni kwa maofisa 179 wapya wa jeshi waliohitimu vyema mafunzo yao mwishoni mwa wiki.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange (kushoto) na Mkuu wa Chuo cha Jeshi (TMA) Monduli, Brigedia Jenerali Paul Massao (kulia) wakimsindikiza Amiri Jeshi Mkuu, Rais Kikwete kwenda uwanja wa Paredi ambapo alitunuku kamisheni kwa maofisa wapya wa jeshi katika sherehe zilizofanyika katika chuo cha jeshi(TMA) mkoani Arusha.

Mkuu wa Chuo Cha Jeshi Monduli (TMA), Brigedia Jenerali Massao, akimsindikiza Amiri Jeshi Mkuu Rais Kikwete kuingia katika viwanja vya Paredi chuoni hapo akiwa katika gari maalumu ambapo alitunuku kamisheni kwa maofisa wapya wa Jeshi.

Amiri Jeshi Mkuu, Rais Kikwete akipokea salamu ya heshima mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Paredi kutunuku kamisheni katika Chuo cha Jeshi Monduli mkoani Arusha, mwishoni mwa wiki.

Amiri Jeshi Mkuu, Rais Dkt. Jakaya Kikwete akikagua kikosi cha Maofisa wapya wa jeshi 

Maofisa wapya wa jeshi wakipita mbele ya mgeni rasmi Rais Kikwete na kutoa heshima wakati wa gwaride maalumu la Kamisheni lilofanyika katika chuo cha TMA Monduli.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru