Wednesday 14 May 2014

70% ya Watanzania wanatumia mitishamba


Na Latifa Ganzel, Morogoro
UGUMU wa upatikanaji wa huduma za afya umesababisha zaidi ya asilimia 70 ya wananchi kutumia huduma za mitishamba.
Hata hivyo, tiba ya miti shamba nchini inakabiliwa na changamoto ya utoaji wa huduma kwa kuwa bado hakuna mfumo wa uchanganyaji dawa makini.
Hayo yalisemwa jana na Mkuu wa Idara ya Matumizi ya Mbao wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine  (SUA), Dk. Suzana Augustino, wakati wa kuwakaribisha Machifu na Maofisa Misitu wa Swaziland, waliokuja nchini kujifunza usimamizi shirikishi wa misitu.
Alisema watu wengi wanakimbilia huduma za matibabu za miti shamba kutokana na urahisi wa upatikanaji wake, pia serikali imeweza kutambua umuhimu wake kwa Watanzania.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Lubombo nchini Swaziland, Sylvia Mthethwa, alisema wamekuja kujifunza usimamizi shirikishi wa misitu kutokana na changamoto ya uharibu wa misitu inayowakabili kwao.
Alisema mafunzo hayo yatasaidia kutunza na kuhifadhi misitu nchini kwao.
“Tumeamua kuja kujifunza Tanzania baada ya kubaini kuwa ni miongoni mwa nchi zinazojitahidi katika uhifadhi wa mazingira,” alisema.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru