Wednesday 14 May 2014

Maiti yaokotwa kituo cha Polisi


Na Latifa Ganzel, Morogoro
MAITI ya Mkazi wa Lubungo Sangasanga, Juma Mbega, imekutwa nyuma ya Kituo Kikuu cha Polisi Morogoro huku baadhi ya viungo vyake vikiwa vimeanza kuharibika.
Mwili wa Mbega (46), uligundulika jana ambapo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Paulo Leonard, alisema polisi walihisi harufu tofauti, walipofuatilia, ndipo wakaikuta maiti hiyo.
Hata hivyo, uchunguzi wa awali wa wataalamu, umebaini kuwa Mbega anadhaniwa kupoteza maisha wiki kadhaa zilizopita.
Inadaiwa kuwa alikuwa na matatizo ya akili na chanzo cha kifo hicho hakijafahamika.
Mmoja wa ndugu wa marehemu, Nuru Adam, aliyefika kituoni hapo, alisema ndugu yake alikuwa na matatizo ya akili na alitoweka nyumbani zaidi ya wiki moja iliyopita.
“Huwa tunafanya naye kazi hapo katika mgahawa wa mama Mangi, wiki iliyopita nilikuwa mapumziko, hivyo sikumwona hadi leo (jana), niliposikia amefariki dunia,’’ alisema.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru