Thursday 22 May 2014

Walimu watakiwa kujisajili mitandao ya pesa


WALIMU wameshauriwa kujisajili katika huduma za M-pesa na Tigo-Pesa, zitakazowaunganisha na huduma za kimtandao za benki wanakopitishiwa mishahara yao.
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba alisema hayo jana alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Sarah Msafiri.
Alisema kujiunga na mitandao hiyo kutawasaidia walimu kurahisisha uchukuaji wa mishahara yao, hasa wale wanaofanya kazi pembezoni mwa miji.
Mwigulu alisema serikali inatambua uwepo na umuhimu wa huduma za kifedha za mitandao ya simu, ambazo zimekuwa zikirahisisha suala la huduma za kifedha kwa wananchi, bila kujali maeneo waliko.
Alisema iwapo walimu watatumia mitandao ya simu za mkononi, iliyounganishwa na huduma za kifedha, wanaweza kupata mishahara yao kwa wakati kupitia simu zao.
ìKwa kuwa malipo ya walimu yanapitia katika benki na kwa kuwa huduma za M-Pesa na Tigo-Pesa kwa sasa zinaunganishwa na mabenki, serikali inawashauri walimu wajisajili na huduma za kimtandao za mabenki wanakopitishiwa mishahara yao ili nao waweze kutumia huduma hizo muhimu,îalisema

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru