Wednesday 14 May 2014

UPL yapata viongozi wapya wa RAAWU


NA KHADIJA MUSSA
WAFANYAKAZI wa Kampuni ya Uhuru Publications Limited (UPL), jana walimchagua Moses Makambi, kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu, Sayansi, Teknolojia, Ufundi Stadi, Ushauri Habari na Utafiti (RAAWU) tawi.
Makambi aliyepata kura 35 aliibuka kidedea kwa kumbwaga mgombea mwenzake wa nafasi hiyo, Hamis Shimye, aliyepata kura 20.
Uchaguzi huo ulifanyika kwa lengo kujaza nafasi zilizoachwa wazi na baadhi ya viongozi ambao wamestaafu, akiwemo Mwadini Hassan, ambaye alikuwa Mwenyekiti.
Mbali na fasi ya mwenyekiti, pia wafanyakazi hao waliwachagua Selina Wilson aliyepata kura 43, kuwa mjumbe wa Kamati ya Wanawake, huku Lilian Timbuka akiibuka na jumla ya kura 46, katika nafasi ya Mwanyekiti wa Kamati ya Wanawake.
Viongozi wengine waliochaguliwa katika mkutano huo wa uchaguzi na kura zao katika mabano ni pamoja na Peter Orwa (45), Kulwa Magwa (37) na Charles Mganga (37), ambao wanakuwa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya tawi.
Awali, msimamizi wa uchaguzi huo, Mariam Mgalula, aliwaasa wajumbe kuhakikisha hawachagui viongozi kwa ushabiki wala kufuata mkumbo, kwa kuwa kitendo hicho kitawagharimu.
Mariam, ambaye ni Katibu Msaidizi wa RAAWU Kanda ya Mashariki, aliwashauri wachague viongozi wenye upeo wa uongozi na wasiokuwa na jazba.
Katika hatua nyingine; baada ya kutangazwa Mwenyekiti, Makambi aliwashukuru wafanyakazi na kuahidi kushirikiana nao katika kuhakikisha changamoto zinazoikabili kampuni zinapatiwa ufumbuzi kwa haraka.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru