Tuesday 20 May 2014

Wazabuni wa chakula magereza kuanza kulipwa


SERIKALI imesema ipo katika mkakati wa kuanza kulipa zaidi ya sh. bilioni 12.3 kati ya sh. bilioni 34.2 za madeni ya wazabuni, ambao wamekuwa wakitoa chakula kwa wafungwa magerezani baada ya fedha hizo kuhakikiwa.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Silima, alisema hayo bungeni jana alipokuwa
akijibu swali la mbunge wa Viti Maalumu (Kagera), Bernadeta Mushashu (CCM), aliyetaka kujua kiasi ambacho wazabuni hao wanaidai serikali na lini fedha hizo zitalipwa.
Silima alisema nia ya serikali ni kulipa madeni hayo yaliyokuwa hayajalipwa kuanzia Julai,
2009 hadi Aprili mwaka huu, kutokana na ufunyu wa bajeti ambayo imekuwa ikitengwa mwaka hadi mwaka kwa ajili ya kutekeleza majukumu ya Jeshi la Magereza..
Alisema wanatarajia kuanza kulipa fedha hizo katika mwaka huu wa fedha 2014/2015.
ìMadeni haya yametokana na ufinyu wa bajeti inayotengwa mwaka hadi mwaka katika kutekeleza majukumu ya lazima ya Jeshi la Magereza. Nia ya serikali ni kuyalipa madeni yote,î alisema Naibu Waziri.
Aliongeza kuwa kwa kuanzia, serikali italipa madeni ambayo tayari yamehakikiwa yanayofikia sh. bilioni 12.3 kati ya sh bilioni 34.2.
Akijibu swali la nyongeza la mbunge huyo, Silima alisema haitawezekana kwa serikali kuongeza kiwango cha malipo kwa wazabuni hao kutokana na madeni yao kukaa kwa muda mrefu.
ìSerikali italipa madeni ambayo wazabuni wameikopesha serikali, japokuwa wazabuni wengi wamefilisika na kupoteza mali zao,î alisema

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru