Friday 9 May 2014

Shule za Tusiime zajizolea tuzo

NA RABIA BAKARI
SHULE za Msingi na Sekondari za Tusiime, zimeng’ara katika tuzo mbalimbali za kitaaluma zilizotolewa na uongozi wa mkoa Dar es Salaam kwa ajili ya shule, wanafunzi na walimu waliofanya vizuri kwenye mitihani ya mwishoni mwa mwaka jana.
Tuzo hizo zilitolewa katika ofisi za Mkuu wa  Mkoa wa Dar es Salaam jana, na Kaimu Mkuu wa Mkoa huo, Raymond Mushi.
Tusiime ziliibuka kidedea kwa kutoa wanafunzi wote walioshika nafasi 10 bora kwa upande wa wasichana na 10 bora wa kiume kwa shule za msingi zisizo za kiserikali.
Pia, ilitwaa tuzo za kufanya vizuri katika masomo yote kwa shule za msingi, na kuingia kwenye 10 bora kwa nafasi mbalimbali kimkoa na kitaifa kwenye matokeo ya shule za sekondari binafsi na nafasi zilizojumuisha shule zote.
Akizungumza baada ya kutwaa tuzo hizo, Mkurugenzi wa shule hizo, Albert Katagira, alisema mafanikio kwa shule yao ya msingi inatokana na kuajiri walimu wenye elimu kuanzia ngazi ya shahada, kitu ambacho si kawaida kwa shule nyingi nchini.
Awali, Mushi alisema vigezo kwa washindi vilitolewa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), kwa kutumia mitihani ya kumaliza elimu ya msingi na kidato cha nne.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru