Thursday 8 May 2014

Mchina afia gesti Dar


NA JESSICA KILEO
RAIA wa China amekutwa amekufa katika nyumba ya kulala wageni ya Euro iliyopo Sinza, jinni Dar es Salaam, alikokuwa amepumzika na mpenzi wake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura, alisema jana kuwa tukio hilo limetokea juzi saa 4:00, ambapo raia huyo Kauma Mgambi Kamiya, alikutwa amekufa kwenye chumba namba 
18.
Alisema kwa mujibu wa wahudumu, Kamiya alifika kwenye nyumba hiyo ya wageni Aprili 4, mwaka huu, akitokea jijini Hong Kong ambapo siku hiyo kabla ya mauti yake alikuwa na mpenzi wake aitwaye Rhobi.
“Kwa mujibu wa taarifa inasemekana marehemu alikuwa akilalamika kuumwa mara kwa mara na alikuwa akipelekwa kutibiwa katika hospitali AAR,” alisema.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru