Wednesday 14 May 2014

Maonyesho ya INGETREX kesho


Na Hamis Shimye
KAMPUNI za kitanzania na wajasiriamali nchini, wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika maonyesho ya kimataifa ya kibiashara.
Maonyesho hayo yanajulikana kwa jina la INGETREX, yanaratajiwa kuanza kesho katika ukumbi wa Diamond Jubilee.
Mkurugenzi wa masoko wa maonyesho hayo, Nuvit Becan, alisema maonyesho hayo ni muhimu kwa Watanzania wanapaswa kuchangamkia fursa.
Alitoa rai kuwa wajitokeze kwa wingi kwa kuwa yatashirikisha watu wa ndani na nje, ikiwemo Uturuki.
“Maonyesho kama haya tumeshayafanya Nigeria, mwezi uliopita na yalikuwa na mafanikio makubwa, ni wakati wa Watanzania kujitokeza kuonyesha bidhaa zao,” alisema.
Kwa upande wake, Balozi wa Uturuki nchini, Ali Davutoglu, alisema uwepo wa maonyesho hayo ni fursa nyingine ya kuonyesha ushirikiano uliopo.
“Tanzania na Uturuki ina ushirikiano mkubwa, hivyo nina matumaini kuwa uwepo wa maonyesho haya utasaidia kukuza uhusiano wa kibiashara kati ya waturuki na Watanzania,” alisema.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru