Wednesday 14 May 2014

Kinara uporajiwa benki atajwa



  • Ni mume wa kigogo wa benki ya Barclays
  • Ana mtandao hatari unaohusisha vigogo

NA MUSSA YUSUPH
POLISI Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, inamsaka Ronald Mollel kwa tuhuma za kuhusika kwenye uporaji wa fedha na mali kwenye mabenki nchini.
Mollel (37), anatuhumiwa kuhusika kupanga njama za kuvamia na kufanya uporaji wa mamilioni ya fedha katika Benki ya Barclays tawi la Kinondoni, Dar es Salaam.
Kamishna wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema jana kuwa mtuhumiwa huyo kwa sasa amekimbilia mafichoni na anaendelea kusakwa kila kona.
Kamishna Kova alidai kuwa Mollel amekuwa akipanga matukio mbalimbali ya uporaji kwenye benki nchini na kwamba, ndiye kinara wa kupanga mikakati.
Kamishna Kova pia alidai Mollel ni mume wa mtuhumiwa Alune Kasililika, ambaye alikuwa Meneja wa Barclays Tawi la Kinondoni wakati uporaji huo ukifanyika. Alune ndiye mshitakiwa namba moja katika kesi ya uporaji huo iliyofunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ambapo anashitakiwa na watuhumiwa wengine
tisa.
Alisema Mollel amekuwa akifanikiwa kufanya uhalifu kwenye mabenki na taasisi za fedha nchini kutokana na kuwa na mtandao mkubwa na hatari unaohusisha watumishi wa benki.
“Mtuhumiwa huyu ni hatari na ana mtandao mkubwa unaohusisha watumishi wa benki mbalimbali, ambao hutumika kufanikisha matukio ya uhalifu nchini,î alisema Kamishna Kova.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru