Thursday 8 May 2014

Jiji la Dar kubadilika


na mwandishi wetu, dodoma
ONGEZEKO la taka ngumu katika Jiji la Dar es Salaam ni moja ya changamoto katika ukuaji na kwamba, jitihada mbalimbali zinaendelea kufanywa. 
Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Hawa Ghasia alipokuwa akitoa mapitio ya kazi zilizotekelezwa kwa mwaka 2013/2014.
Ghasia alisema, katika mwaka wa fedha wa 2013/2014 serikali ilifanya upembuzi yakinifu na usanifu wa miradi iliyobuniwa kuendeleza jijini humo.
Alisema moja ya changamoto zilizo jionyesha ni pamoja na ongezeko la taka ngumu, ujenzi holela wa makazi, usafiri na usafirishaji.
Waziri huyo alisema, halmashauri zote nne za Mkoa wa Dar es Salaam zimehusika katika kutayarisha mapendekezo ya miradi ya kipaumbele itakayotekelezwa kwa kushirikiana na wananchi.
Aliitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na ukarabati wa barabara za mitaa na barabara kuu za usafiri wa mabasi yaendayo haraka.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru