Wednesday 14 May 2014

Wakazi Nyamagana wamshangaa Wenje


NA BLANDINA ARISTIDES, MWANZA
BAADHI ya wakazi wa Jiji la Mwanza,  wamemshangaa Mbunge wa Nyamagana, Ezekia Wenje, kwa kushindwa kueleza faida za kuwepo kwa kikundi cha Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).
Hatua hiyo imetokea baada ya Mbunge huyo wa CHADEMA ambaye ni mmoja wa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, kuacha shughuli zake bungeni na kwenda Mwanza kufanya mkutano wa hadhara.
Wenje ambaye alijinadi uwanjani hapo kwa kutoa lugha za kashfa kwa madai kuwa anahamasisha wananchi kuhusu mchakato wa katiba unaoendelea nchini na uwepo wa UKAWA.
Mkutano huo ulifanyika juzi katika eneo la Dampo jijini hapa, ambapo alieleza kuwa UKAWA walijitoa bungeni kwa madai kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) haiungi mkono Rasimu ya Pili ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, hivyo hawako tayari kuendelea na bunge hilo.

“Tunashindwa kuelewa UKAWA wanalenga nini kwa Watanzania, kwani hata kinachozungumzwa hapa hakina maana, kama katiba ni ya Watanzania, UKAWA ndio wanawatetea, kwanini wasitetee wakiwa bungeni,” alihoji Helman Madoke, kwenye mkutano huo.
Naye Pius Mafuru, alisema UKAWA inawakomoa wananchi wala na si kuwatetea.
Alisema Katiba hiyo si ya vyama vya siasa wala Serikali, bali ni ya Watanzania wote.
Christina Michael, alisema Wajumbe wa katiba hawatakiwi kuonyesha chuki zao za kiitikadi wanapojadili masuala ya wananchi.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru