Wednesday 18 September 2013

Lukuvi aipa maagizo NFRA




SERIKALI imeiagiza Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), kuzingatia ubora na usafi katika ununuzi wa mahindi.
Imesema mahindi hayo yananunuliwa kwa ajili ya chakula kwa Watanzania, hivyo ni lazima yawe na ubora unaokubalika.
Hayo yalielezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, wakati akizungumza na watendaji wa wakala huo katika ziara ya kukagua vituo vya mahindi.
Katika ziara hiyo Lukuvi alikagua vituo vya Mtenga, Namanyere na Kasu vilivyopo wilayani Nkasi, ambapo alipokea taarifa ya ununuzi wa mahindi katika vituo hivyo.
ìItakuwa sio vyema kununua mahindi ambayo yako chini ya kiwango na yaliyo na uchafu mwingi kwa kuwa yananunuliwa kwa matumizi ya chakula ni si vinginevyo. Ni lazima yawe masafi na yenge viwango bora kwa walaji.
ìMwaka huu serikali imetoa bei nzuri ya sh. 500 kwa kilo kwa kuzingatia uhitaji, kutokana na bei hiyo NFRA inatakiwa kununua mahindi yaliyo safi ili kuweza kupanga viwango tofauti ambavyo vitawasaidia katika uuzaji,íí alisema.
Alisema mwaka huu, serikali ndio mnunuzi mkubwa wa mahindi nchini na NFRA ndiyo inayoongoza katika ununuzi huo, hivyo kuagiza kuanza usafirishaji wa mahindi kwenda mkoani Shinyanga mapema kabla kipindi cha mvua kuanza.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru