Tuesday, 3 September 2013

Rais Kikwete kuongoza mamia kumzika Kulola


NA PETER KATULANDA, MWANZA
RAIS Jakaya Kikwete, leo ataongoza mamia ya waombolezaji katika mazishi ya Askofu Mkuu na Muasisi wa Kanisa la EAG (T), Mhashamu Askofu Dk. Moses Kulola.
Mazishi ya Askofu Kulola yanafanyika katika Kanisa la EAG (T), Bugando baada ya mamia ya waombolezaji kutoka kila kona ya jijini hapa na mikoa mingine, kumaliza kutoa heshima zao za mwisho jana, kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.
Mkuu wa Mkoa, Mhandisi Evarist Ndikilo, alisema kuwa Rais Kikwete atakayewasili asubuhi jijini hapa, atahudhuria mazishi hayo ambayo yatafanyika, saa saba mchana, kabla ya kwenda nchini Uganda, kukutana na Rais wa nchi hiyo, Yoweri Museveni.
“Mheshimiwa Rais Kikwete kwa heshima na taadhima atashiriki mazishi ya Mhashamu Askofu Mkuu wa EAG (T) marehemu Moses Kulola kabla ya kwenda Uganda.
“Lakini Uongozi wa Mkoa na Kamati ya Ulinzi na Usalama tunaenda sasa (jana mchana) kuaga mwili wake katika uwanja wa CCM Kirumba,” alieleza mkuu huyo.
Akizungumza katika maombolezo hayo jana, Askofu wa EAG (T), Kanda ya Ziwa Mashariki, John Mahene, alisema katika uhai wake, marehemu Kulola alikuwa akisema yeye ni wa watu wote, Wakristo na wasio Wakrito, na kwamba watu  wanapoomboleza kifo chake wasifanye kama mazoea, wamuenzi kwa mema aliyohubiri.
“Isaya 57:1-2 inasema mwenye haki hapotei… anaondoka asipatikane tena tusikose kutafakari, hivyo Mungu amempumzisha na matatizo ya uzee wa miaka 86, wenye haki wanaenda kupumzika shangilieni…,” alisema kuwaambia waombolezaji.
Naye Katibu wa EAG (T), Ujenzi Makao Makuu, Kadini Lucas, akisoma wasifu wa marehemu, alisema alizaliwa mwaka 1928 katika familia ya Samuel Maguha Kulola katika kijiji cha Nyanonge wilayani Kwimba na kupata elimu ya msingi Ibindo wilayani humo kati ya mwaka 1946 - 1949 na elimu ya kati Bwiru Boys mwaka 1951.
Lucas alisema baada ya kuhitimu masomo ya uchoraji wa ramani za majengo na ujenzi wa barabara, aliajiriwa katika Halmashauri ya Mji wa Mwanza, kabla ya kuacha kazi mwaka 1962.
Alisema alianza utume Juni 2, 1946, saa tatu usiku, wakati wakila chakula na nduguze baada ya kusikia sauti ya Mungu ikimwita mara tatu.
Alisema marehemu Kulola ambaye ameacha mjane, watoto 10, wajukuu 42 na vitukuu 16, alifariki Agosti 29, mwaka huu, katika Hospitali ya Ami jijini Dar es Salaam, baada ya kulazwa hospitalini hapo Agosti 28, kutokana na kuzorota kwa afya yake kulikosababishwa na ugonjwa wa mapafu na moyo.
Katika hatua nyingine, Mkuu wa Mkoa, Mhandisi Ndikilo, akitoa salamu za rambirambi kwenye uwanja huo, alisema marahemu Kulola alikuwa kiongozi bora wa familia, mpenda amani na kwamba ndiyo maana alishirikiana na serikali kulinda amani kwa kuihubiri kwa vitendo ndani na nje na kumshauri mara kwa mara afanye kazi kwa kulinda amani ya wana-Mwanza.
Alisema kama ni suala la kero za muungano nyingi zimeshatatuliwa na kwamba wao msimamo wao ni muungano wa serikali mbili.
Add here…
“Vijana wasijidanganye kwamba serikali tatu zitakuwa na unafuu… serikali tatu ni kuongeza mzigo kwa wananchi, hivyo gharama za kuendesha serikali ya tatu bora ziende kwenye shughuli za maendeleo ya vijana kwa kufungua benki itakayotoa mikopo nafuu kwa vijana,” alisisitiza.
Katika hatua nyingine, Mapunda alisema ameridhishwa na uteuzi huo na kuahidi kuendelea pale alipoishia aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja huo, Martine Shigela.
Awali, Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Dar es Salaam, Omary Matulanga, alisema watampa ushirikiano wa kutosha katibu mkuu mpya ili aweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, kwani wana imani naye, hasa kutokana na rekodi yake ya uongozi mzuri.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru