Wednesday, 11 September 2013

Rufani ya Lissu kusikilizwa leo


Na Mwandishi Wetu, Dodoma
JOPO la Majaji watatu wa Mahakama ya Rufani Tanzania, kesho litaanza kusikiliza rufani dhidi ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, (CHADEMA).
Kwa mujibu wa ratiba za vikao vya mahakama hiyo, rufani hiyo itasikilizwa na Jopo la Majaji Salum Massati, Engela Kileo na Natalia Kimaro.
Rufani hiyo iliyokatwa na Shaaban Seleman na wenzake wawili dhidi ya Lissu, itaanza kusikilizwa saa tatu asubuhi.
Seleman na wenzake, walikata rufani kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, ambayo ilitupilia mbali kesi ya uchaguzi waliyoifungua kupinga ushindi wa Lissu.
Hata hivyo, kabla ya kuanza kusikilizwa kwa rufani hiyo, jopo hilo la majaji linatarajiwa kusikiliza pingamizi zilizotolewa na upande wa wajibu rufani (Lissu).
Akizungumza na waandishi wa habari Mjini Dodoma jana, Lissu, alisema wakati wa usikilizwaji wa rufani hiyo, atawasilisha hoja saba za kuipinga.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru