Tuesday 3 September 2013

Maelfu ya wahitimu kidato cha sita kujiunga na JKT


VIJANA 41,341 waliomaliza kidato cha sita, watakwenda kuhudhuria mafunzo ya kijeshi kupitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa mujibu wa sheria.
Awamu ya kwanza ya vijana hao ilianza Machi, mwaka huu na wamemaliza Julai, mwaka huu.
Awamu ya pili inatarajia kumalizika mwezi huu na ina vijana 10,000.
Kauli hiyo ilitolewa jana bungeni na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Naodha, alipokuwa akijibu swali.
Vuai, alisema mafunzo hayo yameanza kutolewa mwaka huu kwa awamu baada ya serikali kurejesha mafunzo hayo kwa mujibu wa sheria.
Alisema katika awamu ya tatu itakayoanza Oktoba, mwaka huu, jumla ya vijana 15,000 na awamu ya nne itachukua vijana 11,341 ifikapo Januari, mwakani na wanatarajia kumaliza mafunzo yao Aprili.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru