Tuesday 3 September 2013

Tutapigania maslahi ya vijana wote -UVCCM


NA KHADIJA MUSSA
UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), umesema utahakikisha unapigania na kusimamia maslahi ya vijana hadharani bila ya kujali itikadi za vyama, kabila wala dini.
Pia, umesema hakuna sababu ya kuwa na serikali tatu kwa kuwa zitaongezea wananchi mzigo kwa kuwapa watu posho na mishahara isiyokuwa ya lazima.
Hayo yalisemwa jana na Katibu wa UVCCM Taifa, Sixtus Mapunda, alipohutubia umati wa wanachama na viongozi mbalimbali wa umoja huo katika hafla ya kukabidhiwa ofisi iliyofanyika makao makuu wa umoja huo, jijini Dar es Salaam.
Mapunda alisema kwa sasa ajenda kubwa ya umoja huo ni kuhakikisha maslahi ya vijana yanasimamiwa bila kujali dini, itikadi wala chama, huku lengo likiwa kuwawezesha kufikia malengo yao kimaendeleo.
ìKuanzia sasa ajenda yoyote inayohusu vijana tutapigana nayo hadharaniÖ lengo ni kuhakikisha kuwa kijana anapata maendeleo kama vile elimu na ajira,î alisema Mapunda.
Akizungumzia kuhusu serikali tatu, Katibu Mkuu huyo wa UVCCM, alisema halina tija na kwamba serikali mbili zinatosha na suala la Tanganyika libaki katika historia.
Mapunda alisema kwa kipindi cha miaka 50, serikali mbili zimeendelea kutawala kwa amani na kwamba changamoto kubwa za Muungano tayari zimeshatatuliwa.
Kutokana na hilo, alisema ni vyema fedha ambazo zingetumika kwa ajili ya kuendeshea serikali ya tatu zitumike kwa ajili kuanzisha benki maalumu ambayoitawawezesha vijana kupata mikopo ya masharti nafuu ili kuwainua kiuchumi.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru