NA EVA-SWEET MUSIBA, SIRARI
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), imezitaka idara za udhibiti za katika mpaka wa Sirari, kufanya kazi uadilifu ili kudhibiti bidhaa zisizofaa kuingizwa nchini.
Imeonya kuwa kinyume cha agizo hilo, watendaji watakaobanika watachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria.
Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Mara, Joseph Holle, alisema kuwa idara hizo zinapaswa kufanya kazi kwa pamoja ili kuhakikisha bidhaa zisizofaa kutoka nchi jirani haziingizwi nchini.
Alisema kuwa uingizwaji wa bidhaa mbovu ndiyo chanzo cha magonjwa hatari, ikiwemo kansa na kwamba, hata ajali za barabarani nyingi zinasababishwa na vipuri bandia.
Mpaka wa Sirari unatajwa kuwa ni miongoni mwa inayotumika kuingiza bidhaa zisizo na ubora, hivyo TAKUKURU imejikita kusaidia udhibiti wake.
Naye Ofisa kutoka TRA, Paulo Mkondokwa, aliomba vibali vyote kupelekwa mpakani ili taasisi husika zifanye ukaguzi.
Wednesday, 17 September 2014
Watendaji legelege TAKUKURU kukiona
07:37
No comments
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Toa Maoni Yako Kwa Uhuru