Na Mwandishi Wetu
MKURUGENZI wa Mambo ya Kale katika Wizara ya Maliasili na Utalii, Donatius Kamamba ametunukiwa tunzo ya kimataifa ya ‘The knight Cross in the Order of Arts and Letters’ na serikali ya Ufaransa.
Tunzo hiyo imetokana na mchango mkubwa alioutoa katika kulinda na kuendeleza urithi wa utamaduni nchini na duniani kwa ujumla katika kipindi cha miaka 33 aliyoitumikia sekta ya malikale ndani na nje ya nchi.
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Maliasili na Utalii, imesema kwa mujibu wa barua aliyoandikiwa Kamamba na Balozi wa Ufaransa hapa nchini, Marcel Escure, mkurugenzi huyo amekuwa mstari wa mbele katika kusimamia na kuendeleza rasilimali za malikale na kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Jumuia ya Kimataifa.
Kamamba atatunukiwa tuzo hiyo na Balozi Escure katika Ubalozi wa Ufaransa uliopo nchini kesho.
Tuzo hiyo ilianzishwa mwaka 1957 kwa kutambua mchango wa wasanii maarufu na waandishi waliochangia kwa kiasi kikubwa kuendeleza sanaa nchini Ufaransa na duniani kote.
Tuzo ya ìThe knight Cross in the Order of Arts and Lettersî hutolewa nje ya Ufaransa mara tatu kila mwaka, chini ya Mamlaka ya Waziri wa Utamaduni na Mawasiliano ya Umma.
Tuesday, 2 September 2014
Mkurugenzi mambo ya kale apewa tunzo
05:36
No comments
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Toa Maoni Yako Kwa Uhuru