Tuesday, 8 July 2014

Afya ya Sheikh Sudi yaimarika


JESSICA KILEO
HALI ya Mkurugenzi wa Taasisi ya Aswer Muslimu Youth Center, kanda ya Kaskazini, Sheikh Sudi Sudi, aliyejeruhiwa kwa kulipuliwa bomu  jijini Arusha inaendelea vizuri.
Sudi ambaye  alilipuliwa na bomu akiwa na mgeni wake Muhaji  Kifea, walihamishiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) wakitokea Hospitali ya Rufani, Mount Meru Arusha.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii jana, Mkuu wa Idara ya Wagonjwa  ya Nje wa MNH, Dk. Juma Mfinanga alisema wagonjwa hao wanaendelea vema.
Dk. Mfinanga alisema  walipokea majeruhi hao wakitokea katika hospitali ya Mount Meru, Julai 5,  mwaka huu,  wakiwa wamevunjika miguu.
Mfinanga alisema majeruhi hao walifikishwa hospitalini hapo na muuguzi wa Mount Meru. Walijeruhiwa usiku wa manane wakiwa wanakula daku.
“Wagonjwa waliovunjika miguu kutokana na bomu  lililolipuka mkoani Arusha wanaendelea vizuri na sasa hivi  wamehamishiwa katika kitengo cha upasuaji, MOI kwa matibabu zaidi,”alisema.
Shekh Sudi na mgeni wake, Kifea, walilipukiliwa na bomu nyumbani kwa kiongozi huyo eneo la Majengo Chini.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru