Tuesday, 8 July 2014

TIB kuendeleza eneo la Magomeni kota


NA MOHAMMED ISSA
HALMASHAURI ya Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam, imesema ujenzi wa eneo la Magomeni Kota, unatarajiwa kuanza muda wowote mwaka huu.
Akizungumza na Uhuru jana, Meya wa Manispaa hiyo, Yussuph Mwenda,  alisema eneo hilo litajengwa nyumba za makazi na sehemu za biashara.
Mwenda alisema tayari Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB), imeonyesha nia ya kuliendeleza eneo hilo.
Alisema  benki hiyo itashirikiana na kampuni nyingine katika kufanya kazi hiyo. Hata hivyo, alikataa kuitaja kampuni hiyo.
Mwenda alisema ujenzi wa eneo hilo utakapokamilika, utalipendezesha eneo hilo na kuonekana kuwa la kisasa.
Manispaa iliwaondoa wakazi waliokuwa wakiishi katika nyumba za kota na kuwalipa fidia. Hata hivyo, Manispaa imesema watakuwa watu wa kwanza kuangaliwa baada ya mradi huo kukamilika.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru