Saturday, 19 July 2014

Kikwete, Dk. Kamani wawakuna wapinzani

NA PETER KATULANDA, BUSEGA
MADIWANI wa Chama cha UDP wilayani Busega, wamempongeza Rais Jakaya Kikwete na Mbunge wa Busega, Dk. Titus Kamani, kwa kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli na kwamba wananchi hawana budi kuwaunga mkono.
Madiwani hao, Safari Jejeje wa Kata ya Ngasamo na James Yagaluka (Badugu), walitoa pongezi hizo kwa nyakati tofauti wakati wa ziara ya Dk. Kamani, ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, ambapo walisema wana imani kubwa na serikali ya Rais Kikwete kwa kuwa imefanya mambo mengi ya maendeleo ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya CCM.
Yagaluka maarufu kama Lukamangubo, alikuwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Busami, ambapo alisema Dk. Kamani na Rais Kikwete wanatekeleza Ilani ya Uchaguzi kwa vitendo na kutokana na kutokuwa na sera ya ubaguzi katika maendeleo, hata yeye amekuwa akitimiza majukumu yake bila kikwazo.
Katibu wa CCM Wilaya ya Busega, Agatha Magonela, alisema kauli za madiwani hao wa upinzani ni mfano na inadhihirisha namna viongozi wa CCM wanavyowajibika kwa wananchi na kuwa, kazi ya upinzani si kupinga kila jambo, kwenye ukweli ni lazima usemwe.
ìDiwani huyo na mwenzake wa Ngasamo ni mfano bora wa kuigwa na wapinzani wengine nchini maana huo ndiyo ukweli kwamba wanatekeleza Ilani ya Chama chetu.

"Ni kweli bila seranzuri za maendeleo na Utekelezaji wa Ilani ya CCM unaofanywa na Mbunge na Rais wetu
hawana jeuri yoyote, CCM oyee," aliitikiwa na wananchi kwa kishindo "Oyee," Huku akimvalisha kofia ya CCM diwani huyo na kumfanya Dk. Kamani na wana CCM wamshangilie kwea shangwe na vigelegele.
Akimpongeza Jejeje, Magonela alisema kwamba ìHata Yule diwani mwenzake wa UDP Ngasamo, naye tunampongeza Rais Jakaya Kikwete na kumkubali kwa uchapakazi, upinzani wa kweli siyo ugomvi, matusi, vita na porojo za uongo, ni pamoja na kuipongeza serikali na viongozi wake wa CCM wanavyochapa kazi,î alisema.
Awali, akifungua mradi wa Maji katika Kijiji cha Manla, Dk. Kamani alimpongeza Lukamangubo kuwa ni mfano wa kuigwa hata na baadhi ya wana CCM, anamtia moyo zaidi wa kutafuta fedha zaidi kwa ajili ya maendeleo ya wana Busega kwani kazi ya Mbunge siyo kukaa tu jimboni.
Katibu huyo alisema anaamini madiwani hao walipotea tu kwenda chama hicho na kuwataka warudi CCM ili washirikiane kikamilifu zaidi na Mbunge wao na kuwaomba wanachama wa CCM wa wilaya hiyo washirikiane kuwarejesha madiwani hao ëwaliopoteaí na Kata zao.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru