Sunday, 20 July 2014

ZIARA ya Kamani wilayani Busega, Mkoani Simiyu.

Mbunge wa Jimbo la Busega, ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Titus Kamani, akishuhudia maji yakitiririka baada ya kukamilika kwa mradi wa maji wa Kijiji cha Manala Kata ya Badugu wilayani Busega. Kulia ni Katibu wa CCM wa Wilaya ya Busega, Agatha Magonela.

Dk. Kamani akimtwisha ndoo ya maji mama mmoja mkazi wa Kijiji cha Manala, baada ya kufungua mradi huo.

Dk. Kamani akikagua msingi wa Kituo cha kulelea walemavu wa ngozi (albino) kinachojegwa katika Kijiji cha Lukungu Lamadi wilayani humo, mbele yake ni Mratibu wa kituo hicho, Mudy Gimonge.

Dk. Kamani akishiriki na baadhi ya wananchi wa Lukungu kusomba tofali za ujenzi wa kituo cha kulelea walemavu wa ngozi (albino).

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru