Friday, 18 July 2014

ZIARA YA WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII MH. LAZARO NYALANDU NCHINI MAREKANI

  1. Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu (kulia) akizungumza na Balozi wa Heshima wa Utalii wa Tanzania nchini Marekani Ahmed Issa juu ya mikakati mbalimbali ya kuvutia watalii wa kimarekani kutembelea Tanzania jana Beverly, Los Angeles.

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (kati) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Heshima wa Utalii wa Tanzania nchini Marekani Bw. Ahmed Issa (kushoto) na Abdul Majid baada ya kupokea taarifa ya mikakati wanayoitumia kutangaza vivutio vya utalii wa Tanzania kwa wamarekani jana Beverly, Los Angeles.

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (kulia) akiagana na Balozi wa Tanzania wa Heshima wa Utalii nchini Marekani Ahmed Issa mara baada ya kumaliza mazungumzo juu ya masuala kadhaa ya kuvutia Watalii wa Marekani nchini Tanzania jana Beverly, Los Angeles.

Mikakati inayofanywa na Balozi wa Heshima wa Utalii wa Tanzania  Ahmed Issa kutangaza utalii ni pamoja na matumizi ya magari yenye picha za vivutio vya utalii wa Tanzania katika miji mbalimbali nchini Marekani ikiwemo California kama inavyoonekana katika picha.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru